Jumatano , 18th Mar , 2015

Kampeni kubwa ya ZamuYako2015 yenye lengo la kuhamashisha vijana kushiriki katika zoezi kujiandikisha kupiga kura, imeendelea kupamba moto ikiendelea kuungwa mkono na wasanii mbalimbali.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Shilole

Safari hii mwanadada Shilole akiongea na vijana hususani wale kutoka Tabora kuwahamasisha kuwa wao
na wanapaswa kupiga kura.

Shilole katika ujumbe wake kwa vijana hao na wengine wote kutoka sehemu mbalimbali Tanzania amesema kuwa, huu ni wakati muafaka wa wao kuacha kulalamika, na kufahamu kuwa kiongozi yeyote yule wanayemuhitaji, njia pekee ya kumpatia nafasi ni kumpigia kura.