Jumamosi , 14th Mar , 2015

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Sophia Mjema ambaye amepata nafasi ya kuhudhuria siku ya kwanza ya maonesho ya Harusi Trade Fair usiku wa jana,

Mhe. Sophia Mjema - Mkuu wa Wilaya ya Temeke

Amesema kuwa Serikali ipo pamoja na wabunifu na wanamitindo wa mavazi, katika kuhakikisha wanaiendeleza zaidi sekta hiyo kitaifa na kimataifa.

Mheshimiwa Mjema kupitia mahojiano yake na eNewz amesema kuwa, milango ipo wazi kupitia wizara husika kwa wabunifu hawa kuleta mitindo yao na kueleza kile wanachotaka kukifanya, na vilevile kubuni bidhaa bora ambazo zinaweza kuwatangaza na kuitangaza nchi nnje ya mipaka yake.