Jumatano , 18th Mei , 2022

Kundi la Sauti Sol kutokea nchini Kenya limepoteza subscribers zaidi ya 2,000 katika mtandao wa Youtube ndani ya masaa 24 baada ya kutangaza watachukua hatua za kisheria dhidi ya chama cha Azimio La Umoja.

Kundi la Sauti Sol

Sauti Sol walikuwa na subscribes 905,000 na sasa wamepungua mpaka kufikia 903,000

uti 

Mei 16 kundi la Sauti Sol kupitia mitandao ya kijamii walitangaza watachukua hatua za kisheria dhidi ya chama cha Muungano cha Azimio La Umoja, ambacho mgombea wake Urais ni Raila Odinga, kwa madai ya ukiukwaji wa hakimiliki, baada ya chama hicho kutumia wimbo wao wa 'Extravaganza' katika kampeni bila makubaliano yoyote kufanyika.

Wimbo huo ulitumika katika siku ambayo mgombea Urais wa chama cha Azimio, Raila Odinga alimtangaza Martha Karua kuwa mgombea mwenza wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu.