Alhamisi , 8th Mei , 2014

Kundi la muziki la Sauti Sol, katika kile kinachotafsiriwa kama ni hasira baada ya video yao mpya ya "Nishike kuanza kupigwa vita na Serikali ya Kenya, wameamua kudai hadharani pesa walizopaswa kulipwa kwa onyesho katika sherehe za miaka 50 ya uhuru.

Sauti Sol

Sauti Sol wameamua kumdai Rais Uhuru Kenyatta moja kwa moja pesa hizi ambazo ni jasho lao, kupitia mtandao wa twitter, ambapo mpaka sasa bado hakuna majibu yoyote kutoka kwa kiongozi huyu wa taifa la Kenya.

Kitendo hiki kwa upande mwingine kimetafsiriwa kama aibu kwa Serikali na Taifa la Kenya kwa ujmla, kwa kushindwa kufanya malipo kwa wakati kwa wasanii hawa, ikiwa ni miezi 6 imepita tangu walipowatumia katika shughuli yao.