Jumanne , 6th Oct , 2015

Msanii wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya Sarah Kiarie ambaye amekuwa hapa nchini kwa ajili ya Tamasha la kuombea Tanzania amani, ameeleza kuwa anaamini kuwa nchi hii itavuka uchaguzi wake kwa amani na hakutatokea machafuko yoyote.

Msanii wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya Sarah Kiarie

Sarah Kiarie amesema kuwa, kutoka nchini kwao Kenya, ana uzoefu wa namna ambavyo machafuko yanaweza kutibua hali ya mambo, huku imani yake ikiweka dhahiri kuwa Tanzania itamaliza shughuli ya kuchagua viongozi wake wa nchi kwa mafanikio bila kutibuka kwa amani kwa namna yoyote ile kutokana na sifa kubwa ambayo nchi hii inajibebea kuhusiana na suala hilo.