Darassa
Akizungumza na EATV Darassa amesema kwa muda sanaa ya Afrika Mashariki imekuwa ikihitaji kitu kitakachoipa changamoto, ili iweze kuwa na ushindani na kuleta ubora.
“Ni kitu kikubwa sana kwa sababu muziki wetu unahitaji changamoto kama hizi ili uweze kukua, mi nafikiri East Africa Radio, East Africa TV sioni sababu za wao kufanya hivyo, lakini kwa kuifikiria sanaa kiujumla na kuangalia jinsi gani inaweza ikawa sababu ya kitu kimoja kupanda ngazi”, alisema Darassa.
Pia Darassa aliendelea kusema kuwa EATV AWARD zitaleta umoja kwa wasanii wa Afrika Mashariki, na kuongeza urafiki na undugu uliopo, pamoja na kwamba muziki wa Tanzania unazidi kukua.
“Mi nafikiri kadri siku zinavyozidi kwenda na dunia inavyozidi ku'change, wabongo tunazidi kufanya vitu vikubwa sana, kwa kitu ambacho mmekiona cha kuziunganisha nchi zote tatu Afrika Mashariki, ni kitu kikubwa kwanza inaongeza urafiki wetu, inadumisha undugu wetu wa sanaa na michezo kuwa kwenye kitu kimoja mpaka sasa, mmefikiria kitu kikubwa sana”, alisema Darassa.