Ijumaa , 6th Jan , 2023

Meneja wa msanii Diamond Platnumz Sallam SK 'Mendez' amezungumzia kipaji na bahati kwenye mziki na kushauri 'Plan B' kama umekutana na suala hilo.

Picha ya Sallam SK na Diamond Platnumz

"Muziki ulivyo unaweza kuwa na talent lakini ukakosa kitu kinaitwa bahati, ushauri wangu kama umefanya muziki kwa muda mwingi na haujakulipa geukia upande wa pili wa management sababu kuna uhaba wa managers wenye upeo na muziki kwenye industry yetu. Happy New Year" - ameandika Sallam SK 

Sallam SK amesimama nyuma ya mafanikio mengi aliyoyapata msanii Diamond kwenye mziki wake.