Alhamisi , 27th Aug , 2015

Star mkongwe wa muziki Afrika, Salif Keita ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuongezewa ulinzi hususan katika nchi ya Tanzania, katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

staa wa muziki wa nchini Mali Salif Keita akiwa na msanii Lady Jaydee

Agizo hilo limetoka hasa kwa wakati huu kukiwa na hofu kubwa ya usalama wao kutokana na mauaji yao kuhusishwa na imani za kishirikina kipindi hiki.

Star huyo ameeleza kuwa, kwa kulizungumzia suala hilo, na kutumia muziki wake pia kufikisha ujumbe, ana imani kuwa ataweza kusaidia kupambana na mashambulizi ya walemavu wa ngozi ambao mara nyingi wahanga wamekuwa ni watoto.

Kauli ya staa huyo ambaye binafsi ni mlemavu wa ngozi inakuja kukiwa na rekodi za kuuawa kwa albino 76 Tanzania kuanzia mwaka 2000, rekodi za Umoja wa Mataifa zikieleza kuwa viungo vyao vimekuwa vikiuzwa kwa dola 600 mpaka dola elfu 75 kwa mwilim mzima.