Jumapili , 6th Dec , 2015

Diwani ambaye pia ni Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe Said Fella au Mkubwa Fella hivi sasa ameendelea kuongeza nguvu akishirikiana na wakazi wa kata yake ya Kilungule jijini DSM.

Diwani ambaye pia ni Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe Said Fella

Fella ambaye baada ya kufurahishwa na jitihada za wasanii wake Yamoto Band ya kuwania Tuzo za Kimataifa za KORA kwa mwaka 2016 katika kipengele cha Most Promising Artists, ameiambia enewz kuwa pamoja na furaha hiyo akiwa kama diwani amesema kuwa ameanza kazi rasmi za kuongeza visima na kurekebisha njia za upatikanaji wa maji kwenye visima na ujenzi mwingine ambao anauweka wazi hapa.

Pamoja na yote Fella hakuacha kutoa pongezi za dhati kwake Rais John Pombe Magufuli kutokana na jinsi anavyojituma na kuwapa matumaini watanzania kutokana na ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za ugombea urais.