
Rosse Ndauka akiwa na mumewe Haffiyy siku ya harusi yao
Tukio hilo la wao kufunga ndoa limefanyika wikiendi hii iliyopita, ambapo ikiwa imepita mwezi mmoja na siku kadhaa tangu Rosse Ndauka alipovalishwa pete siku ya Machi 2, 2020.
Kupitia post zao wawili hao wameandika kuwa, "Allahmdulilah basi ndiyo hivyo Mrs Mkongwa tena, na ndoa inaraha yake bwana aaaaga mume wangu nakupenda" ameandika Rose Ndauka.
"Akhsante Allah na mimi nimepata utulivu sitochoka kukushukuru, ndoto zangu zimetimia juu ya hili jambo, naamini mengi mazuri yanakuja wewe ni kiboko yangu na kuanzia sasa eti unavimbaa kuitwa mama Mkongwa" Haffiyy.
Rosse Ndauka anaungana na mastaa wengine wa kike ambao wapo katika ndoa kama Shilole, Mayasa Mrisho, Mboni Masimba na Shamsa Ford ambaye ameingia na ametoka kwenye ndoa.
Aidha msanii huyo aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mzazi mwenziye Chiwambo Bandawe ambapo walibahatika kupata mtoto mmoja.