Rosa Ree upande wa kushoto, na Shilole upande wa kulia
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Rosa Ree amesema wakati anakua aliona ukatili huo kwa mama yake akifanyiwa na baba yake jambo ambalo linamuathiri kwenye maisha yake hadi kwa ndugu zake.
"Niliona tukio lile Instagram kiukweli limenisikitisha sana, nimepata uzoefu wa kuona ukatili kwenye mahusiano japo hayakuwa yangu ila ni kwa wazazi wangu najua inavyokuwa kwa mwanamke kupitia kitu kama kile, nilikuwa namtizama mama yangu ni kitu ambacho kimeathiri maisha yangu kwa ukubwa sana kuanzia kwangu hadi kwa ndugu zangu"
Pia Rosa Ree ameongeza kusema "Imenisikitisha sana ila ajue hatakiwi kuwa na mtu ambaye anamnyanyasa, kumtesa au kumfanyia kama vile anatakiwa aione thamani yake anastahili vikubwa zaidi, kuna muda wanawake tuna thamani kubwa sana ila hatujui"
Zaidi tazama kwenye video hapa chini.

