Ijumaa , 2nd Aug , 2019

Mwanadada anayefanya vizuri kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Rosa Ree 'Goddess Of Rap' amefunguka kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na msanii Timmy Tdat wa Kenya.

Rapa huyo wa kike amesema hayo kupitia EATV/Radio Digital baadaya kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Timmy Tdat, ambapo amesema,

Timmy Tdat hajambo ila shemeji yenu mimi simfahamu, ni kazi kama mnavyoweza kuona hakuna hata siku moja mkatuona tuko pamoja kiundani, kingine ni washkaji sana, mimi nina mahusiano mengi ya M\Mungu, familia yangu, kazi na sina muda wa kuwa na mahusiano mengine ya aina yoyote

Wawili hao wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ya siri kutokana na ukaribu walikokuwa nao, muda mwingi walionekana pamoja, kupiga picha na pia kusafiri pamoja.

Rosa Ree na Timmy Tdat walianza kuonekana wakiwa pamoja mwanzoni mwa mwaka huu wakiwa nchini Kenya na Tanzania. Pia aliwahi kusema bado hajapata mwanaume wa kuwa naye.