Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Roma Mkatoliki azua taharuki

Ijumaa , 11th Aug , 2017

Rapa Roma Mkatoliki amewaacha njia panda mashabiki wake kwa kile alichokiimba katika wimbo wake mpya wa 'Zimbabwe' ambapo watu wengi wameshindwa kutafsiri mashairi yalitumiwa humo huku wengine wakiangua vilio baada ya kuona video hiyo.

Rapa Roma Mkatoliki.

Katika wimbo huo Roma Mkatoliki amejaribu kuhusisha matukio mbalimbali ya kisiasa pamoja na lile la kwake kubwa la kutekwa ambapo hii ndiyo kazi yake ya kwanza tokea ule mkasa wake wa kutekwa kuisha na kusababisha maumivu mengine makali kutoka kwa mashabiki zake baada ya kuona 'video' yake mpya iliyojaa hisia kali za maumivu.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa 'youtube' alioweka video hiyo mpya watu zaidi ya 668 wametoa maoni yao jinsi walivyoupokea ujio mpya wa Roma na hizi ni baadhi tu ya zile zilizoandikwa na mashabiki wa Roma.

Pharergy Ramson: "Roma ukienda Zimbabwe harakat atazifanya nani 'but' ngoma iko poa hujawahi kuniangusha ila umebadirika kidogo mzee. Nadhan kwenye hii ngoma umejibu maswali ya watu wengi sana kipindi unafanya 'show' pale 'Dar live' nilitamani urudie hii nyimbo 'but' sikuwa na uwezo ila umefanya vizur."

Blandina Bilau: "Simjui sana Roma wala kufuatilia nyimbo zake lakini huu wimbo umeniliza, 'message' imefika jipe moyo. Mtetezi wako Mungu aendelee kukutetea"

Arthur Oyaro: "Duuh 'so sad' na utu uzima huu machozi nimeshindwa kuyazuia,'thank' pia kwa kunifikirisha. Viva Roma viva''

Mdachi Classic: "Nimefatilia 'comment' nyingi sana ila sijaona hato komenti inayozungumzia vibaya hii ngoma zaidi ni za upendo na za kuumizwa tu. 'In short' hii imetugusa sana pole sana kaka yupo mungu hakimu wa yote".

Ibrahim Utenga: ''This song reflects the real prevailing situation, it's very sensitive song, congratulations to you brother, God save you "

Ndongo Nyambalya: "Nina wasiwasi wewe Mkatoliki hicho siyo kichwa ni semi-computer,  kwenye Mungu wa John na Daud hapo nimefikiria hadi najikuta nurudiarudia kusikiza, U deserve bro! Gat u! 100".

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki amemwagiwa sifa kedekede na mashabiki zake ambao walikuwa wamemisi kusikia na kuona kazi zake kwa kipindi kirefu tokea alipopatwa na mkasa wa kutekwa miezi michache iliyopita na kuweza kurudi katika uhalisia wake bila ya kuhofia jambo lolote litakaloweza mtokea tena mbele yake kwa ukali wa tungo zilizojaa za kufikirika.

HABARI ZAIDI

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea