Picha ya Msanii
Wimbo huo ulirekodiwa katika studio za msanii na mtayarishaji wa muziki marehemu Abel Motika (Mr. Ebbo) huko mkoani Tanga na aliwashirikisha Kassim na Dickson Msami ambaye aliimba korasi (chorus) katika wimbo huo.
Dickson Msami ambaye kwasasa ni mtangazaji wa East Africa Radio na Tv ndiye aliyempeleka studio za Motika kipindi hicho nakulipia gharama hizo kwa ajili ya kurekodi wimbo licha ya kuwa haukuwahi kutoka.


