Roba ambaye aliamua kugeukia shughuli nyingine za kifamilia pamoja na biashara huko Pwani ya Kenya Malindi, amesema kuwa muziki hauwezi kuiacha damu yake, na sasa ambapo mambo yake ya biashara na familia yamekaa juu ya mstari, ameona kuwa ni muda muafaka wa kurudi katika gemu.
Msanii huyu alitoweka katika ramani ya muziki mara baada ya kundi la Kleptomaniax kusambaratika na kila msanii kuanza kushughulika na kazi zake binafsi, na taarifa za ujio wake mpya tayari zimeibua chachu na hamu mpya ya kusikia ladha atakayorejea nayo.