Jumanne , 30th Dec , 2014

Msanii wa muziki wa Bongofleva Ray C ambaye amekuwa katika wakati mgumu kwa kipindi kirefu kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya amekuwa akijitahidi sana kuwashawishi vijana kuhusiana na vita dhidi ya matumizi ya madawa hayo.

msanii wa miondoko ya bongofleva Ray C

Ray C ameongea na eNewz akielezea kuwa tangu alipokuwa akipatiwa matibabu katika taasisi inayoshughulika na waathirika wa madawa hayo, bado amekuwa akipata mtazamo hasi kwa baadhi ya watu kutokana na yeye binafsi kuwa mhanga wa matumizi ya madawa hayo.