Alhamisi , 19th Feb , 2015

Msanii wa muziki Ras Six ambaye anafanya kazi na bendi ya walemavu ya Tunaweza, amesema kuwa anajivunia ubunifu waliowekeza na kutengeneza wimbo wa kuhamasisha amani.

Ras Six

Amesema anajivunia wimbo huo uliowezesha bendi yao kuibuka na ushindi wa pili katika mashindano ya amani yaliyoandaliwa na Busara Promotions.

Ras Six amesema kuwa, Tunaweza Band imeweza kugusia masuala muhimu yakiwepo kuhamasisha watu kuipenda Amani, kukemea vita kati ya wakulima na wafugaji, kusisitiza upendo na kuhusia wanasiasa kuepuka aina yoyote ya uchochezi hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.