Staa wa muziki wa miondoko ya reggae nchini Ras Six
Ras Six ambaye ni mume wa msanii wa kike Irene Malekela kutoka kundi la walemavu la wanadada watatu liitwalo Survival Sisters ameonyesha kujitolea huko akishirikiana na viongozi wake kupitia kituo chake cha 'Shika Mkono Albino Aid in Tanzania'.
Ras Six ambaye hivi sasa anatamba na video yake mpya iliyobatizwa jina 'Mbilimbi' ameiambia eNewz kuwa kituo chake kimeweza kuwafikia watoto mbalimbali nchini na huu ukiwa ni mchango wake mkubwa kwa jamii kutokana na mafanikio yake anayopta kupitia muziki.