Rama Dee
Star huyo wa muziki ambaye kwa sasa ana rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina Usihofiwe Wachaga, ametoa angalizo pia kwa vijana hawa kutokuchukua maamuzi yoyote 'kimizuka', bali kuzingatia zaidi kuwa na hoja za msingi katika maamuzi yao.
Kwa kauli hii Rama Dee anaungana na kampeni kubwa ya "Zamu Yako 2015" inayoendeshwa na EATV na East Africa Radio 'kukusanua' kijana kuwa Usichukulie Poa, jiandikishe na hakikisha kuwa mwaka huu unakuwa sehemu ya maamuzi kwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwisho wa mwaka.