Jumanne , 26th Mei , 2015

Wasanii wa muziki Radio na Weasel kutoka nchini Uganda, kwa mara nyingine tena wamelazimika kuzungumza kukanusha tetesi za kutengana baada ya uvumi mpya kusambaa hivi karibuni kuwa umoja wao utavunjika ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.

Radio & Weasel

Mastaa hawa wamesema kuwa, wamekuwa wakisikia tetesi za kutengana kwao kama watu wengine ambavyo wanasikia, na habari hizi zimekuwa zikivuma mara kwa mara kwa kipindi cha miaka 10 sasa, wakati wao wakiendelea kufanya kazi na kutengeneza pesa.

Radio na Weasel wamekazia kuwa, kwa sasa wanaendelea kupiga kazi bila kujali maneno, katika siku za usoni wakiendeleza mpango wao wa kufanya kolabo na wasanii wa kike katika orodha yao akiwepo Juliana, Desire Luzinda, Leila Kayondo na Irene Ntale kati ya wengine.