Jumatatu , 2nd Jun , 2014

Baada ya ugomvi mkubwa ambao umeyumbisha jina la Radio na Weasel kwa kiasi fulani, wasanii hawa waeonesha mshikamano na kujituma katika kazi na kufanikisha onesho lao mjini Kigali Rwanda kwa mafanikio.

Moze & Radio watua nchini Rwanda Kigali

Radio na Weasel licha ya misukosuko, wamewapatia mashabiki ndani ya jiji la Kigali, onyesho la aina yake wakionyesha nguvu na ushirikiano wa kutosha katika kulishambulia jukwaa.

Kwa sasa Moze bado anafanyiwa uchunguzi kufuatia tukio la ugomvi wake na Jeff Kiwa, ambapo mchakato ukikamilika huenda staa huyu akafunguliwa mashtaka ya uharibifu wa mali na kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi.