Alhamisi , 15th Feb , 2018

Msanii wa Bongo Fleva Rachel aliyetamba na vibao vyake vingi ikiwemo Kizunguzungu, nashukuru umerudi amefunguka na kukana tetesi za kutoa mimba ya TID na kusema hajawahi kushika wala kuwa karibu kimahusiano na TID.

Rachel amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga na moja kwa vijana EATV badala ya kuwepo tetesi za muda mrefu, zikidai mrembo huyo walikuwa wana-share shuka moja na mnyama TID mpaka kupelekea kubebea ujauzito na kuutoa.

"Why TID, Sijawahi kuwa na ujauzito wa TID wala kudate nae, sijawahi kuwa karibu nae kimapenzi na haitakuja kutokea sidhani. Mimi bado sijaamua kuwa mama kwa maana kuna vitu nahitaji nimalize ili niwe mama lakini sina tatizo la uzazi hata siku moja", amesema Rachel.

Kwa upande mwingine, Rachel amedai hata kama angekuwa ameshika ujauzito usingeweza kuwa wa TID kutokana na yeye kuwa na mahusiano na mtu mwingine huko arabuni alipokuwa.

Mtazame hapa Rachel akifunguka mengine zaidi.