Jumatatu , 6th Oct , 2014

Rapa kutoka Kenya, Rabbit a.k.a Kaka Sungura amezungumza juu ya mpango wake kuwa anaachia ngoma mpya kila mwezi kutoka Julai mwaka huu na kusema kuwa hiyo ni kutokana na kuanza mwaka akiwa kimya sana.

Rabbit

Rabbit amesema kuwa, kwa sasa ameamua kuwamwagia ladha tofauti mashabiki wake mpaka atakapofunga mwaka, na pia akaweka wazi juu ya kutua nchini Tanzania hivi karibuni kufanya video ya moja ya kazi hizi.

Rabbit sambamba na hili, akaweka wazi pia mpango wake wa kutua Bongo hivi karibuni kwaajili ya mpango wa kutengeneza video ya ngoma yake inayokwenda kwa jina Najipendelea aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na G Nako.