Jumanne , 15th Jul , 2014

Msanii Rabbit wa nchini Kenya amesema kuwa pamoja na kwamba yeye ni muumini wa dhehebu wa dini ya kikristo lakini ameamua kushirikiana na waumini wa dini ya kiislam katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

msanii Rabbit wa nchini Kenya

Msanii huyo anayefahamika pia kwa jina la Kaka Sungura ameelezea kuwa yeye binafsi ame kua na waumini wa dini hiyo na anaamini hiki kitakuwa kipindi maalum kwake kuweza kuweka mambo yote kando na kushiriki mfungo huo mwezi mzima.

Hivi sasa Rabbit ametoa kichupa chake kipya kilichobatizwa jina 'Nishazoea' ambacho tayari kimeanza kushika chati kwa kasi.