Jumanne , 9th Mei , 2017

Msanii Quick Rocka amefunguka na kudai kuwa wimbo wa 'Bullet' ulimpatia umaarufu mkubwa katika kipindi ambacho alikuwa hajawa tayari kufanya muziki, na kusema akiwa na umri wa miaka 20 alifanya show nyingi kiasi cha kuminyia kapuni zingine.

Quick Rocka anasema alijipatia umaarufu kwenye Hip Hop ya Tanzania kwa hit single yake, Bullet ambayo ilimpa sifa ya kuwa rapa  anayerap kwa kasi zaidi katika muziki wa Bongo hali ambayo ilikuwa inafanya Show kwa upande wake kutokauka mpaka kufikia.

“Every weekend I was booked,” Na kuna time nilikuwa nazunguka sana mpaka nachoka, mpaka sometimes kuna show nazibonyeza, yaani mwili unagoma. Bullet ilinifanya mtu ambaye niko leo, Maisha yalibadilika kwa kasi na kujikuta akiwa busy kila wikiendi kwa show ambazo hazikuwa zikikoma."- amesema Quick Rocka

Hata hivyo Quick Rocka ambaye anajiita 'Switcher' kwa sasa amesema kwamba mafanikio ya Bullet ndiyo leo yamemfanya kuwa mmiliki wa 'Switch Music Group' baada ya kuwekeza kwa kununua vifaa akiwa anafanya kazi na Manecky.

“Kipindi hicho nafanya kazi na Manecky, nilianza kununua vyombo taratibu, ili kuepuka kuombaomba, there is this day nilikuwa naumwa, Manecky na Tudd wakaja kunicheck home, wameingia chumbani kwangu wakakuta nina maspika, mixer, everything wakasema ‘yaani wewe unaumwa halafu una studio ndani!’ nikasema bado nataka nipige building fulani wakasema hizi hizi, usitafute hela zingine, hizi zitakuletea hela ujenge studio, so you have to start with this.’ Walinipush sana kusema ukweli na I have to thank them Manecky na Tudd na nakumbuka kompyuta ya kwanza ya Switch alinipa Manecky.”- Rocka alimaliza