Ijumaa , 15th Aug , 2014

Msanii Quick Racka, ama Switcher kama anavyotambulika sasa, amesema kuwa baada ya kumiliki studio yake mwenyewe, mpango wa kuwasaini wasanii kwa upande wake upo lakini sio kwa sasa kutokana na kazi hii kuhitaji kujipanga zaidi.

msanii wa muziki nchini Quick Rocka

Rapa huyu amesema kuwa, mpango wake katika hili unaweza kuanza mwaka ujao ambapo anatarajia kuanza na msanii mpya ambaye hajawahi kusikika kabisa katika anga za muziki hapa Bongo.

Vile vile wakati mpango huu ukiwa katika mchakato, Quick Racka akagusia suala la mkataba wake na MJ Records ambapo amesema kuwa wanaendelea kama kawaida huku akipata sapoti kubwa kutoka kwa Master J mwenyewe.