Jumanne , 2nd Dec , 2014

Rapa Quick Rocka ameamua kuwatafsiria mashabiki wake maana nzito nyuma ya ngoma yake mpya ya Bishoo featuring Young Dee, akielezea licha ya muonekano mzuri wanaokuwa nao, huwa wanatafuta pesa yao katika mazingira magumu.

msanii wa miondoko ya bongofleva Quick Rocka

Quick Rocka amesema kuwa, wazo hili amelitengeneza akiwa na producer wake Bano, na wameamua kufanya hivi kuwaelezea mabishoo katika mtazamo wa kisasa kabisa, na kutoa rekodi hii ambayo ndani yake rapa huyu amebadilika kwa kiasi kikubwa na kuwekeza pesa ya kutosha, na hapa anaeleza mwenyewe zaidi.