Ijumaa , 14th Mar , 2014

Promota Kim Ueno ambaye mwaka jana alimuingiza matatizoni msanii Iryn Namubiru na kumsababishia kukamatwa na dawa za kulevya huko Japan, amekamatwa na kuwekwa kizuizini kwa uhuma za kupatikana na dawa hizo za kulevya.

Kim aliachiwa huru nchini Uganda baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumfunga kutokana na kosa hili, ambapo katika maelezo yake aliweka wazi kuwa alibeba mzigo huo bila kufahamu ni dawa za kulevya kwa maelekezo ya Kim, kauli ambayo ni wachache walimuamini kwa wakati ule.

Kwa sasa Iryn ana kila sababu ya kufurahi hasa kutokana na tukio hili la kukamatwa kwa Kim kutoa picha halisi ya aina ya mtu ambaye Iryn alikuwa akifanya naye kazi.