Ijumaa , 20th Mei , 2016

Msanii Black Rhino ambaye pia ni kaka wa msanii na Mbunge wa jimbo la Mikumi Profesa Jay, amesema wananchi wa Mikumi kumpata Profesa Jay kuwa mbunge wao ni zawadi toka kwa Mungu

Black Rhino ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, na kusema kuwa kaka yake huyo ni mchapa kazi na mwenye kujituma kuwatumikia wananchi wake.

“Nadhani Mwenyezi Mungu amewapatia zawadi kubwa sana wananchi wa Mikumi kwa kuwapa Profesa Jay kuwa mbunge wao kwa miaka mitano hii ya sasa hivi, kwa sababu ni jembe, anafanya kazi iliyotukuka”, alisema Black Rhino.

Pia Black Rhino amesema naamini kaka yake huyo atawania awamu nyingine na kushinda pia, kwani anamuamini kwa utendaji wake.

“Lazima awakilishe muda wake aliopangiwa pale miaka mitano, na nina hakika ataenda miaka 10, miaka mitano ijayo baada ya miaka mitano hii atashinda kwa sababu ya utendaji wake wa kazi na mambo makubwa ambayo ameanza kuwaonyesha”, alisema Black Rhino.

Profesa Jay amabye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Mikumi.