Jumatatu , 4th Aug , 2014

Rapa Professa Jay, amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, video ya Kipi Sijasikia imekwishakamilika, na ameahidi kuwa itaonekana kwa mara ya kwanza kabisa kupitia Ting'a namba moja ya vijana EATV.

rapa Prof Jay wa nchini Tanzania

Hatua hii ni kwaajili ya kuwapatia mashabiki Afrika Mashariki nafasi ya kuwa wa kwanza kabisa kuona kazi hii ambayo amewekeza nguvu kubwa kabisa ndani yake kuitayarisha.

Pia Jay amesema kuwa hivi sasa anajiandaa kufanya kazi mpya na Chameleone na amepanga utaratibu mpya wa kutoa kazi kwa sasa atakaokuwa akiachia mawe juu ya mawe kwa mtindo alioutambulisha kama Back 2 Back.