Ijumaa , 6th Mei , 2022

Mwandaaji wa filamu ya Binti Seko Shamte, amesema kwamba anadhani hata waandaaji wa filamu wa nje ya nchi siku hizi wamechoka kwani wamejikuta wakirudia kuandaa filamu zile zile ama kuandaa filamu ambazo ni rahisi kutabirika.

Mwandaaji wa filamu ya Binti, Seko Shamte

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 6, 2022, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa TV, wakati akizungumzia kazi zake pamoja na changamoto kubwa ya bajeti za kuandaa filamu zinazowakabili waandaaji wengi.

"Kuwa na bajeti ya kuweza kutekeleza yale yaliyopo kwenye akili yako, hiki ndiyo kitu tunachokipigania sana, halafu pia nadhani producers wengi walioko Hollywood wamechoka, story zao zinajirudia sana, zinatabirika, siku hizi mpaka wanafanya part 1 hadi 7 au wana-redo zile filamu za zamani," amesema Seko