Jumatatu , 31st Mar , 2014

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido ameweka historia nyingine baada ya onyesho lake lililokuwa limepangwa kufanyika huko Brooklyn, New York mwishoni mwa wiki, kujaa kupita kiasi, jambo lililopelekea Polisi kuzuia kufanyika kwake.

Davido

Kuzuiwa kwa onyesho hili la Davido, kumekuja kuwa habari mbaya kwa umati wa mashabiki waliojitokeza kukosa burudani, na vile vile kwa upande mwingine limekuwa kama ishara nzuri ya kukubalika kwa msanii huyu kutokana na mahudhurio kuwa makubwa kuliko ilivyotarajiwa hapo awali.

Davido kwa sasa bado yupo huko nchini Marekani kwa ziara yake kubwa ya kimuziki ambayo pia itamfikisha pia huko Canada kwa ajili ya kuwarusha mashabiki wake.

Tags: