nyota kinda wa kudansi nchini Uganda Patricia akiruhusiwa baada ya kupata matibabu hospitalini
Kisa chake kinda huyo nyota wa kudansi kinaendelea kugusa watu wengi wakiwepo nyota wa kimataifa ambao wamejitolea kumsapoti.
Msimamizi wa Patricia, Eddy Kenzo ameshukuru watu wote waliojitolea kwa namna moja ama nyingine kumsaidia Patricia, akiweka wazi kuwa bili yake ya Hospitali imesimamiwa vizuri na wasamaria, kukiwa na msaada mkubwa pia kutoka kwa nyota wa soka wa kimataifa Emmanuel Adebayor ambaye ameguswa na kumchangia Patricia.
Wakati huo huo, Kenzo ambaye yupo katika kipindi kigumu kwa sasa ameahidi mashabiki zake pale atakapokaa sawa kihisia, ataachia kazi mpya inayokwenda kwa jina Soraye aliyoifanya huko LA Marekani.