Mpacha Peter Okoye na Paul Okoye wanaounda kundi la P-Square
Wimbo umetoka chini ya jina la Peter Okoye na ni wimbo wa R&B, pia taarifa zinazidi kusambaa kuhusu kutoelewana kwa wasanii hawa wawili Peter na Paul wa P Square.
Ikiwa mapacha hawa hapo awali walizoeleka kufanya kazi kwa pamoja huku siku za hivi karibuni kuwepo kwa tetesi za mapacha hwa kutengana, Walianza kutupiana maneno kwa njia ya mtandao haswa baada ya Peter kusema hamtaki meneja wao ambaye ni kaka yao.
Lakini Peter ambaye ndiye ametoa wimbo wake binafsi aliomba radhi kwa kutomtaka kaka yao awe meneja wao kwakuandika "I am not perfect i make mistakes, and it hurts people. But when I say sorry I mean it. I am so SORRY for my actions. I sincerely apologize".
Swali limebaki, je, mapacha hawa wametengana katika kazi zao za muziki? Na ni vipi wataweza kusimama kwa kufanya kazi moja moja!