Jumatano , 9th Jul , 2014

Kaka wa wasanii nyota wa kundi maarufu la P Square nchini Nigeria Jude Okoye yupo mbioni kufunga pingu na mchumba wake anayejulikana kwa jina Ifeoma Umeokeke mnamo tarehe 17 mwezi huu.

Meneja wa P Square Jude Okoye

Jude Okoye ambaye ni kaka yao mkubwa na meneja wa kundi hilo alimvisha pete ya uchumba mchumba wake huyo mwezi Aprili mwaka huu ambapo wamepanga kufanya harusi ya kimila nyumbani kwao Jude, katika mji wa Nnewi, jimbo la Anambra nchini humo.

Sherehe yao kubwa ya harusi (white wedding) itafanyika baada ya mchumba wake Jude atakapojifungua.

Kwa kifupi tu familia hiyo ya akina Okoye inakamilisha orodha huku ikikumbukwa kuwa Peter Okoye ndiye aliyeanza kufunga ndoa na mpenzi wake Lola Omotayo mwezi Novemba mwaka jana, Paul Okoye alifunga ndoa na Babay mama wa Anita Isamah mwezi Machi mwaka huu.