Jumapili , 9th Mar , 2014

Baada ya mafanikio ya muigizaji Lupita Nyong'o kutwaa tuzo maarufu za Oscar katika kipengele cha muigizaji bora msaidizi wakenya zaidi wazidi kung'ara katika sherehe za utoaji tuzo huko Lagos nchini Nigeria.

Katika hafla ya utoaji tuzo za filamu waigizaji wakenya wamefanikiwa kutwaa tuzo 4 kati ya 5 kutokana na uigizaji na ushiriki wao mahiri kupitia filamu iliyoshika chati ya Nairobi Half Life.

Waigizaji hao ni Mohammed Zain, Barbara Minishi ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Art Director, pia wamo Njoki Muhoho, Christian Almesberger na Elayne Okaya.