Alhamisi , 20th Aug , 2015

Star wa muziki wa kike wa nchini Tanzania Nuru The Light ambaye amekuwa kimya katika gemu ya muziki ameibuka tena akiwa tayari kuwapa mashabiki wake ujio mpya wa kazi yake aliyoipa jina la 'L'.

Staa wa muziki wa kike wa nchini Tanzania Nuru The Light

Nuru ambaye hivi sasa ni mjasiriamali na mwanaharakati anayejishughulisha katika kazi za kuwasaidia akina mama kupitia taasisi inayoitwa 'Single Mothers', ameongea na eNewz kuwa ukimya wake huo umetokana na shughuli hizo kuchukua muda wake na hapa anaongea zaidi kuhusiana na ujio wake mpya.