Jumatatu , 17th Feb , 2014

Nyota imezidi kung'aa kwa muigizaji nyota wa nchini Kenya Nini Wacera ambaye hivi sasa amekula mkataba mnono wa kuigiza Nollywood nchini Nigeria.

Nini aliyewahi igiza sehemu ndogo ya filamu maarufu Nairobi Half Life amewahi kuonyesha umahiri wake katika filamu mbalimbali zikiwemo Kona, Dad's Can Cook, Nairobi Law na nyinginezo nyingi.

Meneja wa nyota huyo Alexandros Konstantaras ameelezea kuwa hii ni njia nzuri kwake Nini kupata nafasi hiyo Nollywood kwani ndio ishara ya mafanikio yake katika tasnia hiyo ya uigizaji.