Upande wa kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kushoto ni msanii Nikki Wa Pili
Sasa kupitia EATV & EA Radio Digital, msanii huyo ametaja vitu alivyoviona kwenye uongozi wa miaka mitano wa Rais Magufuli, ambapo hii leo amelivunja rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Kuna vitu ambavyo amevifanya na havikuwepo kabla ya hapo, kwa mara ya kwanza kumekuwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, tulikuwa hatunaga hiyo wizara, pili kumetokea msukumo wakutengeneza umoja wa Taasisi kutoka COSOTA na BASATA, mwanzo COSOTA ilikuwa ipo Wizara ya Biashara na BASATA ilikuwa Wizara ya Habari, tatu kumekuwa na mchakato wa kutengeneza sera mpya ya sanaa na burudani ambayo itatizama kama biashara" ameeleza
