Jumatatu , 8th Mei , 2017

Msanii kutoka kundi la Weusi, Nickson Simon 'Nikki wa II' ametoa ushauri kwa mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi kubaini chanzo kilicho sababisha ajali ya wanafunzi pamoja na walimu katika korongo la Rhotia Marera, Karatu siku ya jumamosi.

Nikki ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa ajali hiyo Mkoani arusha iliyopelekea  jumla ya watu 36 kufariki wakiwemo walimu, wanafunzi na dereva wa shule ya Lucky Vicent Academy

kupitia ukurasa wake wa Instagram Nikki ameandika kwamba,

"Lakini baada ya mazishi lazima uchunguzi ufanyike, kujuwa hali ya gari lenyewe ilikuwaje, maadili ya dereva, na hali ya usimamizi/ukaguzi wenyewe ulikuwaje..... na hii ichukuliwe kuweka udhibiti kwa watu wote walio chukuwa dhamana ya kulea watoto kwa maana ya shule...uthibiti, usimamizi..... haswa katika mazingira haya ya biashara"- Nikki wa II.

Huu ndio ujumbe wa Nikki aliouandika.