Alhamisi , 7th Oct , 2021

Mr poz kwa poz Ommy Dimpoz ameshtua watu kwa kauli yake akimzungumzia Alikiba baada ya kusema hata akimkuta na mkewe atamsamehe kutokana na wema aliomfanyia.

Picha ya pamoja ya Alikiba na Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz amesema hilo wakati wa 'Album Listening Party' ya Alikiba iitwayo 'The Only One King' iliyowakutanisha mastaa kadhaa wa Bongo na nje ya nchi waliopata mialiko ya kuhudhuria kusikiliza ngoma zinazopatikana kwenye Album hiyo.

Ommy Dimpoz anasema anaukumbuka wema wa Alikiba kwa kumsaidia na kuwa naye karibu wakati anasumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Zaidi mtazame Ommy Dimpoz akizungumzia hilo.