Nikki Wa Pili akiwa ndani ya Studio - East Africa Radio
Msanii wa muziki Nicki wa Pili na MwanaFA wameweza kupata nafasi ya aina yake kuonesha uwezo wao wa juu wa kufikiri, na hii ni kupitia kipindi cha Radio cha The Cruize cha East Africa Radio ambacho kilimualika Nicki kama Mtangazaji ambaye alipata nafasi ya kumhoji maswali MwanaFA.
Katika kipindi hiki, kati ya maswali mazito ambayo Nicki alimwuliza FA, ni lile la Ni mambo gani makubwa matano angebadilisha endapo angepata mamlaka kutawala ulimwengu, swali ambalo MwanaFA alikiri linahitaji kukaa na kufikiri na si swali la kutoa majibu papo kwa
papo.
Kwa upande wake Nicki, akilitolea majibu swali hili amesema kuwa angekuwa na Mamlaka ya kutawala Ulimwengu Angebadilisha watu kuwa na Uwezo wa juu wa kufikiri, Mfumo wa wenye kipato kusaidia wasio na kipato, pamoja na swala la haki, huku akisema mengine atayajibu katika mitandao.
Wasanii hawa wawili wamefanikiwa kujiendeleza kielimu hadi kujipatia shahada ya uzamili na wote watakuwa juu ya jukwaa la Kili Tour Kigoma Kesho.