Jumanne , 10th Nov , 2015

Msanii wa Bongo fleva , Mr Nice amesema kuwa hawezi kubadili mtindo wa maisha yake ikiwepo unywaji pombe hadi kulala bar na ametaka watu waelewe kuwa maisha yake hayaingiliani na muziki wake.

Mr Nice

Mr Nice ambaye amekuwa akikabiliana na misukosuko ya maoni tofauti, afya kati ya mambo mengine, amesema kuwa hakuna mtu hata kutoka familia yake ambaye anaweza kutembelea nyota yake hasa sanaa yake ya muziki.

Nyota huyo pia kupitia mahojiano pekee aliyofanya na Planet Bongo amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa yupo sawa sawa kimaisha, akiendelea kutengeneza pesa, akiwa pia anamiliki nyumba binafsi iliyopo Kibamba Dar es salaam.

Star huyo pia ameweka wazi juu ya matayarisho ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina 'Kioo', ambayo inaeleza namna anavyokihusudu kifaa hicho na kukichukulia kama rafiki wake wa kweli aliyebakia, na hapa anaeleza juu ya kazi hiyo.

Sikiliza Sauti ya Nice hapa;