Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Ngoma ya Darassa haina ujumbe"

Ijumaa , 13th Jan , 2017

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Prince Dully Sykes amesema wabongo wengi hawapendi nyimbo zenye ujumbe wa kuhamasisha maendeleo, na ndiyo maana ngoma nyingi zisizokuwa na ujumbe wa aina hiyo ikiwemo ya 'Muziki' ya Darassa, huwa zina hit zaidi.

Darassa

Dully alizungumza hayo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, alipokuwa akizungumzia mikakati yake kwa mwaka 2017 na kutakiwa kuelezea maana ya ngoma yake ya 'Inde' ambayo ilikuwa 'hit' mwaka 2016.

Alisema wimbo wa Darassa hauna ujumbe wowote wa kuhamasisha maendeleo isipokuwa umejaa majigambo na kujisifia, na kwamba nyimbo za aina hiyo ndizo hupendwa na watanzania huku akisema kuwa endapo Darassa angeimba maendeleo, wimbo wake usingependwa.

"Kwani wimbo wa darassa una ujumbe gani? siyo simba, siyo chui, hiyo si ni kujisifia tu, wabongo ukiwaimbia eti sijui twende tukalime, tufanye kazi maendeleo na vitu kama hivyo hawavipendi" Alisema Dully.

Alisema kwa kutambua hivyo, ndiyo maana na yeye hawezi kutunga nyimbo zenye ujumbe wa maendeleo na ataendelea na ngoma kama ilivyo 'inde' na nyingine ambazo zimetikisa anga la bongo fleva

Dully

Hata hivyo, Dully alimpongeza Darassa kwa kazi nzuri na kwa kulishika game la bongo kwa kipindi hiki, na kukiri kuwa kazi yake ni nzuri huku akikataa kuwa ngoma ya Darassa haijamfunika kwa kuwa ngoma yake ya 'inde' ilikuwa hit kabla ya 'Muziki' ya Darassa.

Kuhusu ujumbe uliomo kwenye ngoma ya 'inde' Dully alisema ngoma hiyo aliitengeneza kwa ajili ya kucheza kuburudisha zaidi maana hicho ndicho watanzania wanachokipenda, huku akikanusha kuimba matusi na kusema "Sijaimba matusi, ni jinsi wewe utakavyoutafsiri na kuuelewa, tuliza akili yako utajua nimeimba nini, vitu vingine havisemwi hadharani"

Kuhusu mikakati yake ya mwaka 2017, Dully amesema muda si mrefu atatoa ngoma nyingine ambayo anaamini itakuwa ni kali zaidi ya 'inde' na kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali