Jumatatu , 21st Dec , 2015

Kundi la muziki la Navy Kenzo baada ya kuchukua wasanii wawili chini ya lebo yao ya The Industry (Rosa Ree na Willdone), wameeleza kuwa ili kuhakikisha wanamudu biashara hiyo mpya, wameweka timu ambayo itakayohusika na usimamizi kazi hiyo.

Navy Kenzo

Nahreel amesema kuwa, kazi zao zinatekelezwa kama timu na ili kuepusha kuzingwa na majukumu, kazi yao ikibakia kuwa ni (ku-supervise) kufuatilia kuhakikisha kila kitu kinaenda kama ilivyopangwa.

Katika stori na eNewz, Nahreel amesema kuwa, huo ni mkakati wao kuhakikisha kuwa mbali na biashara ya muziki wanayofanya, wananyanyua vipaji pia.