Jumatano , 27th Mei , 2026

Msanii wa Hip Hop kutoka Afrika Kusini Nasty C amesema kuwa Wizkid ndiye msanii aliyefungua milango ya muziki wa Afrika kwenda kimataifa kwa kiwango kikubwa zaidi, hasa baada ya kufanya kazi na rapper maarufu duniani Drake.

Pichani ni wasanii Wizkid na Nasty C

Akizungumza kwenye moja ya podcast aliyofanya hivi karibuni, Nasty C alieleza kuwa ushirikiano wa Wizkid na Drake uliufanya muziki wa Afrika, hususan Afrobeat, kuanza kupata ufuatiliaji mkubwa kutoka kwa wasanii pamoja na mashabiki wa muziki nchini Marekani.

 

Kwa mujibu wa rapper huyo, mafanikio ya nyimbo walizoshirikiana Drake na Wizkid yalibadilisha mtazamo wa dunia kuhusu muziki wa Afrika na kusaidia kufungua soko kubwa la kimataifa kwa wasanii wengi wa bara hilo.

 

Drake na Wizkid wamewahi kufanya kazi pamoja kwenye nyimbo kadhaa zilizotikisa duniani ikiwemo “Come Closer,” “One Dance” pamoja na “Ojuelegba Remix” ambayo haikuwahi kutolewa rasmi lakini ilipata attention kubwa kutoka kwa mashabiki wa muziki duniani.

 

Ushirikiano huo unaendelea kutajwa kama moja ya hatua muhimu zilizochangia kuukuza muziki wa Afrobeat na kuupeleka kwenye level ya kimataifa iliyoonekana hivi sasa.