Alhamisi , 17th Apr , 2014

Baada ya muda kupita tokea msanii wa muziki Iryn Namubiru alipotengana na baba watoto wake, raia wa Ufaransa Frank Morell, staa huyu kutoka nchini Uganda amesema kuwa hayupo tayari kujiingiza katika mahusiano mengine rasmi na mwanaume kwa sasa.

Iryn Namubiru

Iryn amesema haya baada ya kuulizwa ha moja ya ndugu zake wa karibu kuhusiana na swala la yeye kuolewa tena, swali ambalo lilionekana dhahiri kugusa hisia za mwanadada huyu na kumkumbusha machungu, huku akionyesha dhahiri kuwa hayupo tayari kutoa taarifa zaidi juu ya swala hili zito kwa upande wake.

Iryn kwa sasa anatajwa kuwa katika ugomvi mwingine wa mapenzi baada ya kugundua kuwa mpenzi aliyenaye sasa, ana mahusiano pia na mwanadada anayefahamika kwa jina Safia Kodet ambaye kwa sasa amegeuka kuwa hasimu wake mkubwa.