Alhamisi , 23rd Jul , 2015

Mtayarishaji na msanii wa muziki Nahreel Mkono, ameeleza namna nafasi hizo zilivyoweza kumfaidisha hususan kimapato baada ya kufanya kazi na wasanii wakubwa kutoka nje ya Tanzania akiwepo AKA na KO wa Afrika Kusini kati ya wengine wengi.

Mtayarishaji na msanii wa muziki nchini Tanzania Nahreel Mkono

Nahreel amefafanua namna anavyowachaji wasanii hao wa nje na kueleza utofauti katika kufanya kazi akilinganisha na wasanii ambao amekuwa akifanya nao hapa nchini, huku akikwepa kutaja moja kwa moja figa za cheki ambazo amekuwa akilipwa kwa sababu za kibiashara.

Maneno mtandaoni sasa hivi ni juu ya ngoma mpya ya Navy Kenzo Ft Vanessa Mdee, GAME, Go check it out.