Jumatatu , 30th Nov , 2015

Msanii Kala Jeremiah amesema anafikiria kuachia video ya wimbo wake mpya na audio kwa pamoja, kwani ana haraka ya kuachia kazi hizo kuliko vile shabiki wake wanavyosubiria.

Kala Jeremia ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachoruswa na East Africa Radio, na kusema kwamba video hizo ziko tayari hivyo anasubiri tu kuziachia.

“Nafikiria kuziachia kwa mpigo, huwa some time naachia kwa mpigo au some time naachia kwa kuangalia na timing, kwa hiyo naweza nikaachia labda audio siku moja siku inayofuata nikaachia video, ntaona imekaaje, mpaka kesho video itakuwa ipo mikononi mwangu tayari, ntakuwa nimeshaichukua kutoka kwa director, ukweli ni kwamba nina haraka hata mi wenyewe, nina mzuka kuliko hata mashabiki mwenyewe kuachia ngoma yangu”, alisema Kala Jeremiah.

Kala Jeremia amesema kama ilivyo kawaida yake kila mwisho wa mwaka, anaufunga mwaka kwa style tofauti hivyo mashabiki wake wakae tayari kwa kuona kazi zake.

“Nikisema soon namaanisha very soon, Kala Jeremiah naufunga mwaka kwa style nyingine ya tofauti, watege masikio na watege macho yao kwenye runinga zao”, alisema Kala.