Ijumaa , 6th Jun , 2014

Msanii Mzungu Kichaa ameamua kuzindua mzigo wa kazi mpya, Extended Play ambayo inakwenda kwa jina Relax yenye jumla ya nyimbo nne kwa njia ya onesho la Live litakalofanyika jijini Dar es Salaam akiwa sambamba na bendi yake ya Bongo Beat.

Mzungu kichaa akiwa na gitaa

Kuhusiana na kazi hii mpya na ujumbe ambao unapatikana ndani yake, Mzungu Kichaa amesema kuwa, katika safari yake kimuziki ameona kuwa huu ni wakati muafaka wa kufikisha ujumbe wa Kurelax ama kutulia.